Baada ya majibizano kadhaa ya watumishi wa Mungu Martha Mwaipaja na Upendo Nkone kwenye mitandaoni, mwimbaji Martha Mwaipaja ametangaza kupumzika kwa muda usiojulikana kufanya muziki huku akitaja matatizo aliyoyapitia ndio sababu.
Hii si mara ya kwanza kwa Martha Mwaipaja kuzungumziwa kwenye mitandao ya kijamii, kuna kipindi alizungumziwa sababu ya kutokumsaidia mama yake,kuna kipindi alizungumziwa kuhusu kuwa na ugomvi na dada yake ambaye pia ni muimbaji wa nyimbo za injili Beatrice Mwaipaja hivyo ameona apumzike kuimba.
Je unaona ni uamuzi mzuri alioufanya msanii huyo?