Moja kati ya sifa bora ambazo Nandy anatakiwa kupewa basi ni kusaidia vipaji kutoka mtaani, siku ya jana ametangaza rasmi kumsaini aliyekuwa msanii wa Chief Godlove 'Pipy Jojo' kwenye lebo yake ya 'The African Princes' huku mashabiki wengi wakifurahia uamuzi wake huo wa kumsaidia binti huyo.
Ikumbukwe kuwa Pipy Jojo atakuwa msanii wa pili aliyetangazwa rasmi kuwa chini ya lebo ya African Princes, msanii wa kwanza alikuwa Yammi kuanzia Januari 20, 2023, hadi walipotangaza kutengana mwezi Mei 2025.
Yammi pia alikuwa ni msanii ambaye anaonyesha uwezo wake kwenye mitandao ya kijamii na hapo ndipo Nandy alipoamua kumsaidia mpaka kuwa Yammi huyu tunayemjua leo,hata Pipy Jojo alikuwa huko huko mtandaoni mpaka alipokutana na Chief Godlove na mpaka leo kukutana na Nandy.
Je upo tayari kwa ujio huu mpya wa Pipy Jojo?