Ahukumiwa miaka 40 Jela kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 days ago
rickmedia: ahukumiwa-miaka-jela-kwa-kosa-kukutwa-dawa-kulevya-683-rickmedia

Mahakama Kuu ya Zanzibar, imemhukumu Hamad Ali Mbarouk (18) kifungo cha miaka 40 jela baada ya kutwa na hatia ya dawa za kulevya.

Katika taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Uhusiano Mahakamu Kuu, imesema hukumu hiyo imesomwa leo Aprili 14, 2026 na Jaji wa Mahakama hiyo, Fatma Hamid Mahmoud.

Kwa mujibu taarifa hiyo, Mahakama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa bila shaka kwamba alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 21 (d) (1) cha sheria namba 8 ya mwaka 21.

"Tarehe 26/07/2023 saa mbili na nusu asubuhi huko Malindi mshtakiwa alikutwa na dawa la kulevya aina ya heroin yenye uzito wa kilo 46.154," amesema.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 64/2023, ilifunguliwa Mahakamani hapo Septemba 25, 2023 ambapo jumla ya mashahidi saba walitoa ushahidi huo.