Wasanii wakubwa wa muziki wa R&B, Chris Brown na Usher, wametangaza rasmi ziara yao ya pamoja ya viwanja vikubwa (stadium tour) iitwayo “Raymond & Brown” (R&B)
Hadi sasa, tarehe na miji ya ziara hiyo bado hazijatangazwa, tangazo hilo limeambatana na video ya matangazo (trailer), lakini halijatoa ratiba rasmi ya maonesho
Licha ya ukosefu wa taarifa hizo, shauku ya mashabiki imekuwa kubwa sana hasa kwa kuwa kumekuwa na tetesi za muda mrefu kuhusu kuwa na tofauti kati yao ambapo walijitokeza na kukana hilo, pia tetesi za ushirikiano kati ya wasanii hawa wawili.