Star Wa Muziki Africa SIMBA Diamond Platnumz Kwa Mara Nyingine Ameendelea Kuisimika Bendera ya Tanzania Duniani Kupitia Muziki Baada Ya Wimbo Wake ‘Komasava’ Kuingia Kwenye Chati Kubwa Za Muziki Duniani Za ‘Billboard U.S. Afrobeat Songs’ Na Kushika Nafasi Ya 39 (Ingizo Jipya/ Wiki ya Kwanza ) .
Wimbo Wa ‘Komasava’ Ambao Ulitoka Rasmi Mei Mwaka Huu 2024 na Hakuna Ubishi Kwamba Sasa Wimbo huo kwasasa unawekwa Katika Kundi La Nyimbo Kubwa Zaidi Duniani Kwa Sasa , Baada ya Kuingia kwenye Charts za BILLBOARDS.
Kutokana na hilo, Diamond anakuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania Kuingia Katika chati hizo Tangu Zianzishwe Mwaka 2022
Fahamu kuwa, chart Za “Billboard U.S Afrobeat” inazihusisha nyimbo 50 za Afrobeats zinazofanya vizuri nchini Marekani kwenye streaming, downloads na mauzo ya kawaida.
Aidha, kupitia orodha hii mpya, ‘Komasava’ Ndio Wimbo Pekee Wa Msanii Kutoka Nchini Pamoja Na Afrika Mashariki Kuingia Katika Chati Hizo. Hivyo Huu Ni Ushindi Mkubwa Kabisa Kwa Muziki Wa ‘Bongo Fleva’ Na Afrika Mashariki Yote Kwa Ujumla Ikiwa Ni Mara Ya Kwanza Tangu Billboard Ya Marekani Ianzishwe Kuwepo Na Charts Za Nyimbo 50 Kutoka Afrika
Wimbo Ulioingia Ni OG, Sio Remix !!