Vincent Kigosi "Ray" ametembelea kaburi la swahiba wake Steven Kanumba

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 hours ago
rickmedia: vincent-kigosi-ray-ametembelea-kaburi-swahiba-wake-steven-kanumba-531-rickmedia

Msanii maarufu wa filamu nchini Tanzania, Vincent Kigosi almaarufu Ray amegusa mioyo ya wengi baada ya kushiriki video akiwa ametembelea kaburi la aliyekuwa msanii mwenzake na rafiki wa karibu, Marehemu Steven Kanumba, katika kuadhimisha mwaka mpya.

Kupitia video hiyo, Ray ameambatanisha ujumbe mzito wa maombolezo akisema:

Leo Ni Mwaka Mpya Nimemtbelea Ndugu Yangu Makaburini kwenda Kumuombea iIli Aendelee Kupumzika kwa Amani….

The Great Ukimya Wangu Huu Sio Kama Sikukumbuki Hapana,

Nakukumbuka Sana Ndugu Yangu Ila Mungu Yaye Alikuhitaji Zaidi Endelea Kupumzika Kwa Amani Ndugu Yangu Ipo Siku Tutakutana Sehemu Nyingine Tofauti Na Hii Tuliyopo Sasa ….

MWANGA WA MILELE AKUPE BWANA NA MWANGA WA MILELE AKUANGAZIE UPUMZIKE KWA AMANI AMEEEN.