Kama ilivyo kawaida kwa wasanii tofauti tofauti wanavyotoa ahadi kuhusiana na mienendo ya lebo zao ndivyo ambavyo Mfalme wa Bongoflava Alikiba alivyotoa ahadi katikati ya mwaka jana 2025 kuhusu lebo yake ya Kings Music kumsaini msanii wa kike, ametimiza ahadi hiyo amemtambulisha msanii wa kike kutoka Rwanda Mutima Wangu.
Kwenye Mahojiano ya Saraphina Jerry na Alikiba mnamo Jul 4, 2025 Alikiba alikuwa akiongelea suala la wasanii Tommy Flavour na K2ga kutoka kwenye lebo ya Kings Music na wasanii pekee waliopo ni Vanillah na Abdukiba na aligusia kuwa kuna msanii mwingine tutamtambulisha hivi karibuni na Saraphina Jerry alipomgusia kwa kumwambia ndiye yule wa kike Kiba alijibu ndio,kwahivyo Mtima aliyetambulishwa dISEMBA 31 2025 ndiye msanii aliyekuwa akitajwa na Alikiba muda wote na anakamilisha idadi ya wasanii 3 kings music.
Tazama hapa chini Interview Hiyo👇🏾