Kutangaza kampuni ya Kamari kwamuweka Drake Matatani,ana kesi

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 hours ago
rickmedia: kutangaza-kampuni-kamari-kwamuweka-drake-matataniana-kesi-224-rickmedia

Rapa Drake na streamer Adin Ross wametajwa kwenye kesi kadhaa za pamoja Marekani zinazolenga jukwaa la kamari mtandaoni Stake.us.

Walalamikaji wanadai Stake.us inaendesha kamari haramu kwa kivuli cha “sweepstakes,” ikiruhusu pointi kubadilishwa kuwa pesa halisi.

Kesi zimefunguliwa Virginia, Missouri na New Mexico. Drake na Adin Ross wanatuhumiwa kutumia ushawishi wao kutangaza jukwaa hilo kwa njia inayodaiwa kupotosha, hasa kwa vijana.

Walalamikaji wanataka fidia ya mamilioni ya dola na kusimamishwa kwa shughuli za Stake.us nchini Marekani. Stake imekanusha tuhuma; Drake na Adin Ross bado hawajatoa majibu.