Rapa Fetty Wap atoka Jela baada ya kusota miaka 3 Jela

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 days ago
rickmedia: rapa-fetty-wap-atoka-jela-baada-kusota-miaka-jela-500-rickmedia

Rapa Fetty Wap amerudi nyumbani rasmi baada ya kutumikia zaidi ya miaka mitatu kati ya kifungo chake cha miaka sita Jela.

Baada ya kuachiliwa, alizungumza na Loren Lorosa wa The Breakfast Club, akieleza shukrani zake, mambo aliyojifunza akiwa gerezani, na nia yake ya kuanza upya maisha na muziki.

Fetty Wap alifungwa jela baada ya kukiri kosa la kuhusika na biashara haramu ya dawa za kulevya na Alikamatwa mwaka 2021 na mamlaka za serikali ya Marekani.

Alishtakiwa kwa njama ya kusafirisha na kusambaza dawa za kulevya, hasa kokaini, Mwaka 2023 alihukumiwa kifungo cha miaka sita gerezani.