Willy Paul atamba kuwa msanii wa Kenya anayetambulika zaidikimataifa

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

13 hours ago
rickmedia: willy-paul-atamba-kuwa-msanii-kenya-anayetambulika-zaidikimataifa-511-rickmedia

Mwanamuziki Willy Paul Msafi anasema mashabiki wa Kenya hawampi maua yake ipasavyo lakini ndio msanii pekee anayetambulika zaidi kimataifa na nyimbo zake zinachezwa sana nje.

Willy Pozze amesema hilo baada ya 'Content Creator' wa Kenya Atruthk kumtaja kama msanii wa kimataifa lakini watu wanamchukulia poa.

"Asante kwa utambuzi, watu wanajua ukweli hawanipi maua yangu ni sawa. Mimi Ndiye msanii pekee wa Kenya ambaye nyimbo zake zinachezwa zaidi kimataifa kuliko wasanii wengi wa hapa".

"Hata msukume watu wengine kiasi gani fact ni Pozze ndio anatambulika huko nje" - ameandika Willy Paul