Wimbo wa Harmonize 'Yanga Bingwa' wafutwa Youtube na Innoss'B

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 year ago
rickmedia: wimbo-harmonize-yanga-bingwa-wafutwa-youtube-innossb-202-rickmedia

Mwanamuziki kutoka Congo Innoss'B Auondoa YouTube wimbo wa Harmonize 'Yanga Bingwa' alioutoa wiki iliopita.

Kwa mujibu wa Innoss'B amesema kuwa kuna mtu ametumia wimbo wake kupeleka mashtaka YouTube kuwa Harmonize ametumia wimbo wake (Innoss'B). Innoss'B anasema kuwa ameshawasilisha jambo hilo kwa wakala anayesimamia muziki wake kuwasiliana na YouTube haraka iwezekanavyo ili kutatua changamoto hiyo.

Kwa upande wa Harmonize amemsifu Innoss'B kuwa ni mtu safi na kuainisha kuwa kuna watu wapo nyuma wanaofanya mchezo huo mchafu.